- Target:
- Wanawake Live ya Joyce Kiria
- Region:
- Tanzania
- Website:
- www.facebook.com
Sisi wanawake wa Arusha tunaomba kwa kupitia muandaji wa kipindi cha wanawake Live, Joyce Kiria atuandalie mafunzo ya wasichana wa kazi kama ilivyofanyika huko Dar.
Tumeona ni mafunzo yenye tija kwa wasichana wa kazi na hata akina mama wenye familia zetu kwa vile kuna mahusiano makubwa sana kati yetu na watu hawa. Tunahitaji kukumbushana majukumu yetu katika kulea familia, mchango wa kila mmoja katika majukumu ya kila siku na zaidi ni kwa jinsi gani tunaweza kuishi kwa kushirikiana na sio kwa kuwindana kama hali ilivyo sasa.
Pia kumsaidia msichana kujitambua masuala ya afya yake na familia hususan watoto ni jambo la muhimu sana. Mafunzo ya kujilinda na afya na pia kujua haki za msingi za wanawake hawa wa kazi pia itatoa fursa nzuri na elimu yenye tija kwa wanawake hawa.
Wote tuliotia sahihi hapa tunaomba Joyce Kiria na timu yake ya Wanawake Live waje hapa Arusha kutoa Mafunzo hayo kwa wasichana wa kazi.
You can further help this campaign by sponsoring it
The Mafunzo ya wasichana wa kazi Arusha petition to Wanawake Live ya Joyce Kiria was written by Carolyn Kandusi and is in the category Residential Disputes at GoPetition.